Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Katambi: Serikali inajivunia kuwa na Waajiri wanaothamini Wafanyakazi


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Patrobas Katambi amesema serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan inajivunia kuwa na Waajiri wanaothamini Wafanyakazi kwa kuwa ni rasilimali pekee yenye kuleta matokeo yanayotarajiwa na Waajiri.

Mhe. Katambi amebainisha hayo leo Aprili 30, 2024 Jijini Dar es salaam wakati wa Hafla ya utoaji Tuzo ya Mfanyakazi Bora (Simba Bingwa) wa mwaka 2024 itakayowawezesha wafanyakazi kuendelea kuchapa kazi kwa bidii na kuhakikisha mahusiano mema yanaimarishwa sehemu za kazi.

Aidha, amewasihi wafanyakazi kuongeza juhudi na maarifa katika kazi ili kuwezesha Kampuni kufikia malengo na kufungua mianya ya ajira kwa watanzania katika kuongeza fursa za ajira nchini.

Sambamba na hayo, amezipongeza Kampuni za Simba kwa kuthamini, kutambua na kupongeza jitihada zinazofanywa na wafanyakazi katika Kampuni hizo na kuandaa tuzo kwa ajili ya kutambua mchango wao.
.