Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Nimeridhishwa na Maandalizi ya Maadhimisho ya Mei Mosi - Majaliwa


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambayo yatafanyika kitaifa mkoani Arusha.

Amesema hayo leo (Jumanne, Aprili 30, 2024) wakati akikagua maandalizi hayo ambayo yatafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha.

“Nimeridhishwa na maandalizi, niwatie shime tukamilishe sehemu iliyobaki, kesho tutakuwa wote, Waziri Mhe. Deogratius Ndejembi yupo na timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu ipo hapa”

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inaridhishwa na ushirikiano uliopo baina yake na vyama vya wafanyakazi nchini na itaendelea kuwajibika kwa yote muhimu yanayowaguswa wafanyakazi “tunazungumza pamoja na kukiwa na jambo lolote tunashirikishana, muelekeo wetu bado ni mzuri”

Awali akitoa taarifa ya Maandalizi hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Deogratius Ndejembi amesema hatua ya kukamilika kwa maadalizi hayo umefanywa na serikali kwa ushirikiana na wadau wa utatu ambao ni ATE, ILO na TUCTA.

Kwa upande wake, rais wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini(TUCTA),Tumaini Nyamhokya ambaye alikuwepo katika maandalizi hayo amesema kuwa kamati za maandalizi zimefanya kazi kubwa sana ikiwemo hamasa katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo. “Mpaka sasa maandalizi yote yamefikia asilimia 95, na hizo tano kwa Saa machache zilizobaki tunakwenda kuyamaliza”

Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.