Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

JESHI LA MAGEREZA NA PSSSF WATAKIWA KUKAMILISHA MIUNDOMBINU YA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI CHA KARANGA KWA WAKATI


Ofisi ya Waziri mkuu imeziagiza Jeshi la Magereza nchini na Mfuko wa hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), zinazotekeleza kwa pamoja mradi wa zaidi ya shilingi bilioni 75 wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga, Moshi, Mkoani Kilimanjaro kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati miundombinu ambayo bado kukamilika ili kiwanda kianze uzalishaji mara moja.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Andrew Massawe, ametembelea mradi huo na kutoa maagizo matatu kwa pande mbili zinazotekeleza mradi huo ikiwemo kuhakikisha vifaa vya umeme vilivyoagizwa kwa kampuni za ndani vinapatikana na mkazo mwingine kuhusiana na ulinzi hususani wa mashine ambazo tayari zimeshawasili kufutia gharama yake kubwa.

Katika Hatua nyingine wakuu wa Taasisi wabia katika mradi huo,wametoa mitazamoa yao kufuatia maagizo ya Ofisi ya waziri mkuu.


Matarajio ya kiwanda hicho cha kimkakati ambacho ni upanuzi wa kiwanda cha sasa kinachozalisha jozi 400 za viatu kwa siku,zikiwemo buti za jeshi na kiraia,ni ,kuzalisha jozi 4,000 za viatu vya kiraia pekee kwa siku sawa na takribani jozi milioni 1.2 kwa mwaka kikiratajiwa kuzalisha jumla ya ajira 7,000. Kwa sasa mradi huo wa ujenzi wa Kiwanda hicho umefikia asilimia 95.