News
Prof. Ndalichako awatahadharisha Wastaafu dhidi ya utapeli wa mtandaoni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Prof Joyce Ndalichako amewatahadharisha wastaafu watarajiwa dhidi ya utapeli wa kimtandao unaofanyika pindi wanapo karibia kustaafu.
Prof. Ndalichako amesema hayo Septemba 11, 2023 Jijini Dar es Salaam katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) iliyolenga kutoa elimu kwa wastaafu hao ili waweze kujiandaa vizuri kabla na baada ya kustaafu.
Amesema kumekuwepo na utapeli kupitia mtandao ambapo wastaafu wamekuwa walengwa wakuu wanaotapeliwa fedha kwa kutuma pesa, taarifa zao binafsi , namba za akaunti za benki na nywira bila kutambua kuwa wanatapeliwa.
Aidha, amewasihi Maafisa Utumishi wa umma kutunza taarifa za watumishi wao na kutozitoa kwa watu wasio stahili.