Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Serikali itaendelea kufungua fursa za Ajira kwa Vijana: Ummy Nderiandanga


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga amesema kuwa Serikali itaendelea kuongeza fursa za ajira kwa vijana na kuweka mazingira wezeshi ili waweze kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.

Mhe. Ummy Nderiananga amesema hayo wakati wa akihitimisha maadhimisho ya siku ya vijana kimataifa tarehe 12 Agosti, 2025 katika ukumbi wa Mabele uliopo Mabeyo Complex, Jijini Dodoma.

Amesema kuwa, vijana ni nguzo muhimu ya maendeleo ya taifa, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana naoi li kuwekewa mazingira rafiki ya kuwawezesha kujiajiri na kuajiriwa.

“Tanzania ina idadi kubwa ya vijana na kati yao wenye umri wa miaka 15 hadi 35 ni asilimia 34.5, kwa kutambua umuhimu wa vijana kama nguvu kazi ya Taifa Serikali ipo tayari kuhakikisha vijana wanawezeshwa ili waweze kufikia malengo yao,” amesema

Aidha, Naibu Waziri Nderiananga amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu inaratibu programu za vijana zinazotekelezwa na Wizara nyingine katika sekta mbalimbali nchini. Pia, programu za uwezeshaji vijana kiuchumi kupitia mfuko wa Maendeleo ya vijana, mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri na mifuko mingine ya uwezeshaji wananchi kiuchumi lengo ikiwa kuwezesha vijana kunufaika na mikopo himilivu itakayowasaidia kuanzisha miradi itakayowawezesha kujiajiri na kuajiri vijana wenzao.

Vile vile, amesema Ofisi ya Waziri Mkuu inaratibu programu ya Taifa ya kukuza Ujuzi kwa vijana ambapo vijana hupatiwa mafunzo ya ufundi stadi, ujasiriamali na stadi za kazi kupitia vyuo vya ufundi stadi vilivyopo nchini. Ameongeza kuwa, Serikali imepanga kuanzisha ‘Skills Development Center for Overseas Employement’ ili kuwasiaida vijana wa kitanzania wanaotafuta fursa za ajira nje ya nchi wanaunganishwa na fursa hizo na wanaweza kumudu ushindani wa soko la ajira.

Kwa upande mwengine, Mhe. Ummy Nderiananga amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa Maendeleo ili kukuza ustawi wao na kuhakikisha malengo ya vijana yanafikiwa.