Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

WAZIRI MHAGAMA AMEKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MENEJIMENTI YA OFISI YA WAZIRI MKUU – KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiongoza kikao cha Menejimenti kilichofanyika hii leo Januari 16, 2020 katika Ukumbi wa Mkutano uliopo Ofisi ya Waziri Mkuu, Ngome Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi (kulia) ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu), Mhe. Ummy Nderiananga.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiongoza kikao hicho alipokutana na Menejimenti kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Ofisi hiyo.

Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ndg. Andrew Massawe (kulia) akitoa taarifa kwa Waziri Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Mawaziri anayeshughulikia (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi (kushoto) na Mhe. Ummy Nderiananga anayeshughulikia (Wenye Ulemavu).

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkutano uliopo Ofisi ya Waziri Mkuu, Ngome Jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu), Mhe. Ummy Nderiananga akieleza jambo wakati wa kikao kazi hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkutano uliopo Ofisi ya Waziri Mkuu, Ngome Jijini Dodoma Januari 16, 2020.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipitia taarifa pamoja na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu), Mhe. Ummy Nderiananga (kulia) wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Ofisi hiyo.

Kamishna wa Kazi, Brig. Gen. Francis Mbindi (katikati) akieleza kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusiana na Sekta ya kazi wakati wa kikao hicho kilichokuwa kikiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama.