Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, akikata utepe wakati akikabidhi magari 30 na vitendea kazi vya kupima afya na usalama mahali pa kazi kwa ofisi za Mikoa za Idara ya Kazi na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa Sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi (Meimosi), iliyofanyika mkoani Morogoro, Mei mwaka huu, hafla hiyo imefanyika Agosti 7, 2023 katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma.