Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Katambi awataka vijana kufanya kazi kwa uadilifu na uadilifu


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amewataka vijana kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu ili kujiepusha na athari za kuwa kwenye kumbukumbu mbaya za utumishi wao.

Aidha, amesema kuwa hali hiyo inakwamisha jitihada za vijana kujikwamua kiuchumi na kushiriki katika ujenzi wa taifa.

Mhe. Katambi amesema hayo Septemba 8, 2023 Bungeni, jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Geita Mjini Costantine John Kanyasu lilihoji, Serikali inatambua utaratibu wa Mgodi wa GGML wa ku-blacklist vijana nchini na ni vijana wangapi wapo blacklisted.

Akijibu swali hilo, Mhe. Katambi, amesema Serikali imewahi kupata malalamiko kuhusu vijana ambao wamesitishiwa ajira zao katika mgodi huo na ufuatiliaji uliofanyika haukubaini suala hilo.

Amesema kilichobainika ni kuwa mgodi huo umeweka utaratibu wa kutunza taarifa za kiutendaji na mienendo ya wafanyakazi wake ikiwemo matendo na matukio ya ukiukwaji wa kanuni na taratibu ambayo mfanyakazi anakuwa amefanya katika kipindi cha ajira yake.

Kwa upande mwengine, Mhe. Katambi amewataka vijana ambao wana uhakika utumishi wao katika Mgodi huo bila dosari na wanaweza kuthibitisha kuwa wamekuwa black-listed, kuwasiliana na Ofisi yake ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.