Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Maelfu ya Vijana kushiriki Maadhimisho ya Wiki ya Vijana


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi - Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema zaidi ya Vijana 1000 wanatarajia kushiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa Mkoani Manyara.

Mhandisi Luhemeja amesema hayo Oktoba 6, 2023 alipofanya ziara Mkoani humo kwa ajili ya kukagua maendeleo ya shughuli za mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2023 na maandalizi ya wiki ya vijana akiambatana na Menejimenti ya Ofisi hiyo.

Aidha, amewasihi vijana kujitokeza kwa wingi katika wiki hiyo ili kujadili fursa zinazozotolewa na serikali na kutatua changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo ukosefu wa mitaji na ajira.

Kwa upande wa Katibu tawala wa Mkoa huo Bi. Karolina Mthapula amempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza kilele cha mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kufanyika Mkoani humo.

Maadhimisho ya wiki ya vijana Kitaifa yanatarajiwa kuanza Oktoba 8 hadi 14, 2023 Mkoani humo ambapo vijana kutoka Tanzania bara na visiwa watashiriki katika wiki hiyo.