Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Katambi Aagiza Uzingatiaji Usalama na Afya Mahali Pa Kazi


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amemtaka Meneja wa Kiwanda cha kutengeneza nguo 21st Centry Tushpvir Singh kuzingatia usalama na afya mahali pa kazi kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Katambi amesema hayo Septemba 20, 2023 alipofanya ziara kiwandani hapo kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria za kazi, ajira na sheria ya afya na usalama mahali pa kazi.

Amesema wafanyakazi kutokuwa na vifaa kinga, mikataba isiyo rasmi, kufanya kazi kinyume na saa za kazi, maslahi hafifu ya wafanyakazi hali ambayo inahatarisha maisha yao.

Sambamba na hayo, amemtaka Meneja huyo kuzingatia kima cha chini cha mshahara kama kinavyoelekezwa katika sheria ya kazi.

“Kuna maeneo ambayo yanazalisha joto kali, kukaa katika maeneo ya joto muda mrefu kuna athari kubwa za kiafya unaweza kuzipata,” amesema.