Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Katambi afungua Michezo ya Mei Mosi Mkoani Arusha


* Amehimiza Wafanyakazi kushiriki michezo ili kuimarisha Afya na kuweka Mwili imara dhidi ya Magonjwa Yasiyoambukiza.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Patrobas Katambi amefungua rasmi michezo ya Mei Mosi na kueleza umuhimu wa michezo hiyo katika kuimarisha afya za wafanyakazi.

"Michezo ni Afya, Ajira na njia nzuri ya kujenga umoja na mahusiano mema mahali pa kazi," amesema

Mhe. Katambi amesema hayo leo Aprili 20, 2024 wakati wa uzinduzi wa michezo ya Mei Mosi Kitaifa inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha.

Aidha, Mhe. Katambi ameeleza kuwa, Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua umuhimu wa michezo kwa wafanyakazi katika kuongeza ufanisi kazini na kukuza maendeleo ya taifa kwa kuwa na nguvu kazi imara.

Kwa upande mwengine, amehimiza Waajiri na Vyama vya Wafanyakazi kuweka msukumo wa wafanyakazi kushiriki katika michezo sambamba na kuruhusu michezo mahala pa kazi.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Mei Mosi Taifa, Bi. Rose Masamu amesema ameipongeza serikali kwa kushirikiana na TUCTA kutambua umuhimu wa wafanyakazi kushiriki katika michezo.

Kwa Mwaka 2024 Michezo ya Mei Mosi inaogozwa na Kauli Mbiu isemayo " Michezo ni Afya na Ajira, Tutunze Mazingira, Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu" Kazi Iendelee.