Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Prof. Ndalichako awakumbusha Viongozi wa Mikoa kuwasilisha madeni ya michango ya Hifadhi ya Jamii


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof.Joyce Ndalichako amewakumbusha viongozi wa mikoa kuhakikisha wanawasilisha madeni ya makato ya michango ya Hifadhi ya jamii ambayo watumishi walikatwa ila haikuwasilishwa kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Mhe Amewasisitiza kutekeleza hilo kwakuwa kutolipwa madeni hayo husababisha usumbufu mkubwa kwa wastaafu ambapo wanacheleweshwa kulipwa haki zao kutokana na michango yao kutowasilishwa na waajiri katika mifuko.

Prof. Ndalichako ameyabainisha hayo leo tarehe 26 Agosti, 2023 wakati wa Mafunzo ya Wakuu wa mikoa na Makatibu Tawala wa mikoa, Tanzania bara, mjini Kibaha mkoani Pwani.

Masuala mengine aliyosisitiza kwq Wakuu wa mikoa ni kuhakikisha wanasimamia Masuala ya ajira na ukuzaji ujuzi, maendeleo ya vijana, Masuala ya Watu wenye Ulemavu,Masuala ya shughuli za maendeleo ya vijana pamoja na Masuala ya kazi.