Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Rais Samia Awahimiza Wananchi Kutunza Mazingira


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itafanya mapitio ya Sera na mitaala ya elimu katika ngazi zote ikiwa ni jitihada ya kuwawezesha vijana nchini.

Aidha, Rais Samia amesema lengo ni kuleta mageuzi makubwa ili elimu inayotolewa kwa vijana iakisi mazingira na mahitaji ya nchi ya maendeleo na kuwawezesha wahitimu kujiajiri na kuajirika kiurahisi.

Rais Samia amesema hayo wakati wa Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Wiki ya Vijana kitaifa katika Uwanja wa Kwaraa.

Kwa upande mwingine, Mhe. Rais Samia amewataka wananchi kutunza mazingira kwa kuwa zaidi ya asilimia 95 ya mabadiliko ya tabianchi yanatokana na shughuli za kibinadamu ambazo zinaathiri misimu ya mvua na kupotea kwa vyanzo vya maji.

Pia, Rais Samia amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuhakikisha bei ya gesi inashuka ili kuhamasisha wananchi wengi zaidi kuacha matumizi ya mkaa ambao unaharibu ikolojia na madhara ya kiafya.