Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Serikali yatenga Sh. Bilioni 9 kutekeleza Programu ya Taifa ya kukuza ujuzi kwa Vijana


Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu imetenga Shilingi Bilioni 9 ikiwa ni bajeti ya kila mwaka kwa ajili ya kutekeleza Programu ya Taifa ya kukuza ujuzi kwa vijana.

Hayo yamebainishwa Agosti 28, 2023 na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ajira na Ukuzaji ujuzi Robert Masingiri alipotembelea Chuo cha Utalii Arusha kwa ajili ya kukagua mafunzo yanayotolewa chuoni hapo.

Amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 tayari serikali imetenga fedha hizo ambapo hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu kiasi cha shilingi Bilioni 5 zimeshatolewa kwa ajili ya kutekeleza Pogramu hiyo.

Aidha, amesema Programu ya Taifa ya kukuza ujuzi inahusika na mafunzo kwa njia ya vitendo, kurasimisha ujuzi mahali pa kazi, mafunzo ya utarajali (internship) na kukuza ujuzi kwa waliopo kazini kulingana na mabadiliko ya teknolojia.