Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wampokea Katibu Mkuu mpya Mhandisi Cyprian Luhemeja


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Mhandisi Cyprian John Luhemeja amewasili katika Ofisi hiyo Jijini Dodoma Septemba 4, 2023 na kupokelewa na Menejimenti pamoja na watumishi wa Ofisi hiyo, ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Katibu Mkuu Luhemeja alikutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi pamoja na Menejimenti ya Wizara hiyo.

Baada ya mapokezi hayo Mhandisi Luhemeja alikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi hiyo inayojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba.