Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kamishina Lilian abainisha vigezo utoaji wa vibali vya kazi nchini



Kamishina wa Kazi Msaidizi - Vibali vya Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Lilian Francis ametoa mwongozo wa vigezo vya kupata vibali vya kufanya kazi nchini kwa raia wa kigeni.

Akizungumza leo Aprili 16, 2024 kupitia mahojiano na Clouds Fm, amesema miongoni mwa vigezo vinavyozingatiwa katika utoaji wa vibali vya kazi kwa wageni ni sifa za Kielimu/Taaluma aliyonayo mgeni, Ujuzi wa Kazi, Uzoefu wa Kazi, manufaa yatakayopatikana kutokana na Taasisi au Kampuni katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi nchini kupitia kazi anayo fanya.

Aidha Kamishina Lililan amebainisha vigezo vingine ni uwiano wa wafanyakazi wazawa na wageni ambapo mfanyakazi 1 wa kigeni anakuwa na uwiano wa wazawa 10 na kuthibitishwa na mamlaka za serikali katika miradi wanayoitekeleza.

Katika hatua nyingine, amesema Ofisi hiyo ina jukumu la kuwezesha wageni kufanya kazi ya uwekezaji nchini kwa mujibu wa kanuni na sheria zilizowekwa.