Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kiongozi Mbio za Mwenge Apongeza Uhifadhi Mazingira


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Ekiakim Mnzava amesema ameridhishwa na utunzaji wa uhifadhi wa mazingira unaotekelezwa katika shamba la Miti la Rongai lilipo Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro ambalo linasimamiwa na Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Amesema hayo April 05, 2024 wakati Mwenge wa Uhuru ulipotembelea na kukagua shughuli za upanda miti katika Shamba hilo pamoja na Uzinduzi wa Kitalu cha miti.

Kiongozi huyo amesema, Mwenge umekuta kitu cha tofauti miti imepandwa, imetunzwa na inakuwa na hilo ndio jambo ambalo wanalifanya Nchi nzima kuhakikisha miti inayo pandwa inatunzwa vizuri na sio kupanda miti na kuitelekeza na kama wapo watu wanataka kujifunza upandaji wa Miti wafike Rombo ili kuweza kuona jinsi gani wanavyo tunza miti waliyoiotesha.

“Mwenge wa Uhuru mwaka huu una lengo la kuelimisha na kuhamasisha Watanzania juu ya utunzaji mazingira, hivyo amewasihi wananchi kushiriki katika uhifadhi wa mazingira ikiwa hatua ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi,” amesema Mnzava

Akitoa taarifa ya Shamba la Miti Rongai kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge, Mhifadhi wa Shamba la miti Rongai Joel Naasi ameeleza kuwa, Shamba hilo lina Bustani ambazo zinauwezo wa kukuza miche laki sita na bustani hiyo imekuwa chanzo kikubwa cha miche inayo pandwa kwenye shamba hilo, sambamba na kugawa kwa jamii na Taasisi za Umma na Binafsi.

“Mwaka wa fedha 2023/2024 Miche 26,900 imegawanywa kwa ajili ya utunzaji wa Mazingira, pamoja na kuoakoa vyanzo vya Maji,” amesema