Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Serikali yapongezwa kuratibu fursa za Ajira nchini


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Fatma Toufiq (Mb) ameipongeza serikali kwa kuratibu fursa za ajira nje ya nchi ambazo zinatoa fursa kwa vijana kuajiriwa na kujiajiri wenyewe.

Aidha, ameishauri serikali kuendelea kutafuata nafasi za ajira katika nchi nyingine zenye upungufu wa ajira ili vijana wa kitanzania wapate nafasi ya kwenda kufanya kazi katika nchi hizo.

Mhe. Toufiq amebainisha hayo Aprili 8, 2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati wa Majadiliano ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2024/2025.

Kwa upande mwingine amesisitiza uwepo mfumo maalumu wa kubaini wafanyakazi wote wanaofanya kazi nje ya nchi ili kufanya ukusanyaji wa mapato kupitia ujira wao.