News
Waziri Ridhiwani akabidhi Vifaa Kinga na Saidizi kwa Wenye Ulemavu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amekabidhi vifaa kinga na saidizi kwa Wenye Ulemavu , Jijini Dodoma.
Mhe. Ridhiwani ametoa Vifaa hivyo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Watu wenye Ulemavu kuhusu kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika kuimarisha utoaji wa huduma na kukuza ustawi wa watu hao iliyoandaliwa na Ikupa Trust Fund.
Aidha, amekabidhi Mafuta ya Saratani ya Ngozi chupa 103 kwa Wenye Ualbino, Magongo kwa wenye Ulemavu wa miguu, fimbo nyeupe, Kofia pana Miwani kwa wenye Ualbino.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mhe. Ridhiwani amesema “Watu wenye Ulemavu ni sehemu ya nguvu kazi ya Taifa, hivyo wanapaswa kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo sawa na wasio na ulemavu, hii ndiyo imekuwa dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan” amesema.