News
Waziri Ridhiwani Kikwete ashiriki Mbio za Mwenge wa Uhuru Monduli
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ameshiriki katika Mbio za Mwenge wa Uhuru wilaya ya Monduli, ambapo miradi mbalimbali imezinduliwa ikiwemo Mradi wa Maji katika kijiji cha Esilalei, Kata ya Mtowa Mbu, Mkoani Arusha.
Aidha, akizungumza Mhe. Ridhiwani amewahimiza wananchi wa Wilaya ya Longido kulinda miundombinu ya maji katika eneo hilo ili kuhakikisha upatikani wa maji endelevu.
Vile vile, amewapongeza wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 kwa uzalendo na moyo wa kujitolea wanaouonyesha katika kuzunguka nchi nzima wakihubiri Umoja, Amani na Maendeleo.
“Kazi yenu si tu ya kihistoria bali ni ya kipekee kwa kuwa inagusa maisha ya wananchi kwa kuhamasisha uwajibikaji, uadilifu na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa ufanisi. Kupitia jitihada zenu, Mwenge wa Uhuru unaendelea kuwa alama ya mshikamano na dira ya mafanikio ya Taifa letu” amesema.
Mradi huo unatarajiwa kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa eneo hilo na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.