News
Waziri Ridhiwani Kikwete: Tanzania Mwenyeji Mkutano wa Kimataifa wa Wadau Sekta ya Hifadhi ya Jamii Afrika
Waziri wa Nchi Ofisii ya Waziri Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji katika mkutano wa Kimataifa wa wadau wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Afrika (ASSA), unaotarajia kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Jijini Arusha.
Akizungumza wandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mhe Ridhiwani amesema kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Dkt.Philip Mpango Julai 10 mwaka huu, anatarajia kufungua Mkutano huo ambapo Mifuko hiyo ya kinga ya jamii itakayoshiri kutoa Tanzania Bara na Zanzibar ambayo ni NSSF, PSSSF, NHIF, WCF, ZSSF na ZHHF.
Aidha, amesema mkutano huo utahusisha ushiriki wa wadau wa Sekta hiyo, kuhudhuria kongamano hilo ambalo litafanyika Julai 09 mwaka huu Jijini humo, ambapo mada mbalimbali zinazohusiana na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii zitajadiliwa kwa kina.
Mhe. Ridhiwani amesema lengo la kongamano hilo ni pamoja na kuwakutanisha wadau, watunga Sera, wasimamizi na watendaji wa Sekta ya hifadhi ya Jamii Afrika ili waweze kwa pamoja kujadili na kuazimia namna Sekta hiyo ilivyokuwa na uwezo mkubwa katika ujenzi wa miundombinu na huduma nyingine za kijamii katika Bara la Afrika.
Jumuiya ya (ASSA) inaundwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutoka Nchi 15 za Bara la Afrika ambazo ni pamoja Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Sudan ya Kusini, Comoro, Cote d'ivoire, Gambia, Sierra Leone, Mali, Namibia na Tanzania ambayo ni wenyeji wa mkutano huo.