Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

Frequently Asked Questions

1.Mtu yeyote kwa niaba ya familia ya marehemu atatoa taarifa ya kifo kwa mwajiri haraka iwezekanavyo. Aidha mtu yeyote kwa niaba ya familia ya marehemu anaweza kutoa taarifa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko haraka iwezekanavyo katika kipindi kisichozidi miezi 12 baada ya kifo ncha mwajiriwa kilichotokana na ajali au ugonjwa uliotokana na kazi.

2.Mwajiri anatakiwa kutoa taarifa ya kifo kwa Mkurugenzi Mkuu ndani ya miezi 12 baada ya kifo cha mwajiriwa kilichotokana na ajali au ugonjwa uliotokana na kazi kwa kutumia Fomu WCN – 1.

3.Mwajiri atapaswa kujaza nakala halisi tatu (3) za Fomu WCN – 1, nakala ya kwanza itapelekwa kituo cha afya au hospitali (Iwapo mgonjwa aliyefariki alikuwa anaendelea na matibabu) Nakala ya pili itapelekwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko na nakala ya tatu itabaki kwa mwajiri. Fomu hizi tatu ziwe na muhuri wa mwajiri

4.Baada ya kutoa taarifa ya kifo cha Mwajiriwa kwa Mkurugenzi Mkuu, Mwakilishi wa familia ya marehemu atatakiwa kujaza taarifa za wategemezi kwa kutumia Fomu WCP – 7 ambayo itathibitishwa na mahakama.

5.Mwajiri au mwakilishi wa familia ya marehemu atawasilisha madai ya fidia kwa Mkurugenzi Mkuu kwa kutumia Fomu WCC-1 na taarifa za wategemezi zilizopo katika Fomu WCP-7 pamoja na vielelezo vifuatavyo:

a)Cheti cha kifo

b)Kibali cha mazishi

c)Ripoti za polisi (taarifa ya askari wa barabarani endapo ajali imetokea barabarani, angani, majini na taarifa ya upelelezi kama kifo kimetokea kazini)

d) Muhtasari wa kikao cha wanandugu uliyoidhinishwa na mahakama husika ambapo shauri la mirathi limefunguliwa

e)Kiapo cha msimamizi wa mirathi

f)Hukumu ya mahakama kuhusiana na mirathi husika

g)Taarifa za kibenki za wategemezi

h)Cheti cha ndoa kama marehemu ameacha Mjane/mgane au kiapo cha ndoa kwa mwenza kutoka mahakamani

i)Nakala za vyeti vya kuzaliwa vya watoto kama marehemu ameacha watoto chini ya umri wa miaka 18

6.Mkurugenzi Mkuu atatoa maamuzi juu ya madai ya fidia ndani ya siku 30 baada ya kupokea madai yaliyokamilika.

(i)Waombaji wanapaswa wawe wanne ama zaidi.

(ii)Taratibu nyingine zinapaswa kuwa kama zilivyokuwa kwa usajili wa chama cha wafanyakazi katika 5.2 (a) hapo juu.