Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Joyce ndalichako, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Dkt. Moses Kusiluka, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) Tumaini Nyamhokya na viongozi wengine wakiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano (Solidarity) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambayo Kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro tarehe 01 Mei, 2023.