Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

Registration of Trade Unions

Ofisi ya Msajili wa Vyama Huru vya Wafanyakazi na Waajiri ni moja ya vitengo vilivyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu.

Ofisi hii ilianzishwa mwaka 2000, baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha Sheria ya Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri Na.10 ya Mwaka 1998, ambayomadhumuni yake ni kuruhusu haki na uhuru kwa wafanyakazi na waajiri kuanzisha na kujiunga na vyama vya wafanyakazi na waajiri kwa hiari yao.

Kabla ya kuwepo kwa vyama vya wafanyakazi na waajiri na mashirikisho tulivyonanvyo mpaka sasa, masuala ya vyama vya wafanyakazi na waajiri walikuwa yanashushulikiwa na chama cha African Commercial Employees Association (ACEA) kilichoaznizwa mwaka 1951.Wakati huo kilikuwa kinaongozwa na Bw.Shaib Seif kama Rais, E.mahiza kama Mwandishi (General Secretary), Bw.Kamaliza MwekaHazina na Bw. Mpangala ambaye alikuwa ni Mwanachama wa Halmashaur ya Chama.


Chama hiki hakikuwa kimesajiliwa kama chama cha wafanyakazi na mnamo tarehe 20 Novemba, 1952 maombi ya kukiandikisha chama kama chama cha wafanyaakazi yalipelekwa serikalini.Hatahivyo maombi hayo hayakukubaliwa. Chama cha Agfrican Commercial Employees Association kilikuwa kikichukua wanaxchama wake kutokana na wafanyakazi waliokuwa wanafanya kazi viwandani au makampuni sio wafanyakazi wa serikali. Wanachama wa kwanza kujiunga katika chama hicho walikuwa ni makarani na hivyo viongozi wake wote walikuwa karani.

Wakati ambapo chama cha African Commercial Employees Associations kilipokuwa kikiendesja kazi zake mawazo ya kuwepo kwa vyama vya matajiri(waajiri) yalifikiwa.Matajiri hao awalikuwa wakiwakataza viongozi wa vyama vya wafanyakzkazi kungia katika viwanda vyao ili kuweza kuzungumza na wafanya kazi na kuwashawishi kuingia katika vyama.Kwa ajili hii maendeleo ya vyyama yalaikuwa polepole na wafanyakazi iwaliogopa kuingia kwenye vyama na wale walioingia na kuwa wanachma hawakuipo ada zao sawa sawa.wakati huo inakadirwa ni wanachama 30 tuu walioweza kulipa ada zao kila mwezi katika chma hicho. Ada ya chama kwa mwezi ilikuwa ni sh1/- kna kiingiliao sh.3/-.


Our Services
Union Registration
Union Registration

Chama chochote kinachoanzishwa kitalazimika kujisa...

How Do I?
  • Ni kosa la jinai kwa chama chochote cha Wafanyakazi/Waajiri kuendelea kufanya kazi za chama bila kuomba kujisajili.
  • Ubaguzi wowote wa kumbagua mtu kwa kuwa ni Mwanachama wa chama cha wafanyakazi/chama cha waajiri unakatazwa chini ya Sheria na atakayefanya hivyoatakuwa ametenda kosa la jinai na kesi hizi zinashughlikiwa katka mahakama za wilaya na za hakimu mkazi.
  • Kusimamia haki na maslahi ya wanachama wake.
  • Kusimamia kikamilifu Katiba za Vyama, Kanuni na Sheria zinazohusika.
  • Kusimamia utekelezaji wa Sheria za Kazi.
  • Kuwawakilisha wanachama wake katika vikao vya kinidhamu.
  • Kuwasilisha taarifa za wanachama na hesabu zilizokaguliwa na Mkaguzi anayetambulika Kisheria kwa Msajili, katika tarehe na wakati uliowekwa na Sheria hii.
  • Kuhakikisha kuwa fedha za chama zinatunzwa vizuri na kwa kuzingatia taratibu za Sheria.
  • Kutunza orodha ya wanachama wake kwa Mujibu wa Sheria na kanuni zake.

Uundaji wa Shirikisho la wafanyakazi/waajiri utahusisha vyama vya wafanyakazi/waajiri vilivyosajiliwa visivyopungua vitano (5), vyenye uhusiano wa karibu.

(i)Waombaji wanapaswa wawe wanne ama zaidi.

(ii)Taratibu nyingine zinapaswa kuwa kama zilivyokuwa kwa usajili wa chama cha wafanyakazi katika 5.2 (a) hapo juu.

(i)Waombaji wanapaswa kuwa 20 ama zaidi.

(ii)Chama kinapaswa kitokane na wafanyakazi wenyewe na kisianzishwe kwa maslahi binafsi.

(iii)Jina la chama halipaswi kufanana na jina la chama kingine kilichosajiliwa.

(iv)Chama lazima kiwe na anwani Tanzania Bara.

(v)Chama kinatakiwa kisiwe na mahusiano ya moja kwa moja na Mwajiri yaani mwajiri asiwaanzishie ama kuwachagulia wafanyakazi chama.