Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kamati ya Bunge yaridhishwa na kasi Ujenzi Chuo cha Wenye Ulemavu Mwanza


*Chuo hicho kunufaisha vijana wenye Ulemavu kupata ujuzi wa Ufundi Stadi.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imetembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Vijana wenye Ulemavu kinachojengwa Bujora, Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Machi 19, 2024, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Fatuma Toufiq amesema Kamati imeridhishwa na ujenzi wa chuo hicho na kupongeza jitihada zote zolizotumika kufanikisha mradi huo.

“Tumeridhishwa na ujenzi wa chuo hiki na tunamshukuru sana Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutambua makundi mbalimbali yenye uhitaji ikiwemo wenye Ulemavu. Hakikaka ujenzi wa chuo ukikamilika utasaidia kuboresha maisha ya vijana wenye Ulemavu", alisema Mhe. Toufiq

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameihakikishia kamati hiyo kuwa ofisi yake itasimamia kwa karibu ujenzi huo ili ukamilike kwa wakati.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi huo imekamilika na awamu ya pili imepangwa kuanza mwaka wa fedha 2024/25 ambapo baada ya kukamilika ujenzi chuo hiko kitaanza kufanya kazi.