Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kikao cha Ushirikiano baina ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji (SMZ) chafanyika Jijini Dodoma


Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu imepata ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar ambao umelenga katika kubadilishana uzoefu katika masuala ya kazi, maendeleo vijana, ukuzaji ajira na ustawi wa Watu wenye Ulemavu.

Ugeni huo umeongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais anayesimamia masuala ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji. Katika kikao hicho ofisi hizo zimedhamiria kushirikiana kwa karibu katika kutekeleza majukumu sambamba na kutoa huduma kwa wananchi kwa tija na ufanisi katika pande zote mbili za Muungano.

Aidha, katika kikao kazi hicho Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Kazi, Uchumi na Uwekezaji aliambatana na Kamishna wa Kazi – Zanzibar pamoja na Mkurugenzi wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSH) – Zanzibar.