Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AAGIZA KUFUTWA KIBALI CHA KAZI CHA MGENI KAMPUNI YA BNBM


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde leo amefanya ziara ya ukaguzi katika Kampuni ya vifaa vya Ujenzi ya BNBM na kubaini ukiukwaji mkubwa wa sheria za kazi hali iliyomlazimu kutoa maagizo makali kwa mwajiri.

Maagizo yaliyotolewa na Naibu Waziri Mavunde ni kama ifuatavyo;


(I) Kamishna wa Kazi kufuta mara moja kibali cha Kazi cha Ndg. HU BIN raia wa China ambaye amekutwa akifanya kazi tofauti na aliyoombewa kibali.

(II)Wafanyakazi wote wa Kampuni ya BNBM ambao hawana mikataba ya kazi kupewa mikataba yao ifikapo Ijumaa tarehe 17.01.2020

(III) NSSF na OSHA kufanya ukaguzi wa kina na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria katika masuala ya Mwajiri kutowasilisha baadhi ya michango ya wanachama katika mfuko wa NSSF na uzingatiaji wa masuala ya Afya na Usalama mahala pa kazi.

(IV)Idara ya Kazi na Uhamiaji kuwahoji kwa pamoja kwa raia 10 wa China ambao wamekutwa kiwandani hapo huku nyaraka zao na shughuli ambazo zimewaleta hapa nchini kuonekana kutoshahabiana.

(IV) Kupigwa Faini ya jumla ya Tsh 5,000,000 kwa waajiri BNBM na Tropical Co. kwa kushindwa kutoa vifaa kinga kwa wafanyakazi ambao wamekutwa wakiwa wanafanya kazi katika mazingira hatarishi.

(VI) Chama cha Wafanyakazi TUICO kufika mara moja hapo kutoa elimu na kusaidia uanzishwaji wa Tawi la Chama cha Wafanyakazi.



Aidha Naibu Waziri Mavunde amewata waajiri wote nchini wanaoajiri wageni kuhakikisha wanafuata masharti ya vibali vya kazi na pia kutekeleza sharti la urithishwaji ujuzi kwa wazawa ili kuwajengea ujuzi na baadaye kurithi nafasi husika.