News
NSSF Kujenga Ofisi 10 za Wilaya kusogeza huduma Karibu na Wananchi
✅Kamati ya Bunge yakagua maendeleo ya mradi wa ujenzi Ofisi ya Wilaya ya Hai
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umepanga kujenga ofisi 10 katika maeneo mbalimbali nchini kwa mwaka wa fedha 2026/2027, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi, wakiwemo wanachama na wajiri wa katika sekta binafsi.
Akizungumza katika ziara ya kikazi ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii ya kukagua mradi wa ujenzi wa Jengo la kitega uchumi pamoja na ofisi ya NSSF Wilaya ya Hai, Novemba 10, 2026.

Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amesema ujenzi wa ofisi hizo ni hatua muhimu katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za Hifadhi ya Jamii kwa urahisi.

Akitoa ripoti ya mradi mbele ya kamati hiyo , Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bwana Masha Mshomba amesema uwepo wa shughuli nyingi za Kiuchumi, biashara na waajiri wengi wa sekta katika eneo hilo la Hai ni sababu zilizopelekea Mfuko kutekeleza mradi huo, huku Meneja miradi wa NSSF ,Mhandisi Helmes Pantaleo akidadavua hatua ya ujenzi iliyofikiwa.

Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi Helmes Pantaleo amesema mradi huo wa ujenzi umefikia asilimia 50 na unatarajiwa kugharimu Shilingi bilioni 9.16 hadi kukamilika kwake.
