Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Prof. Ndalichako asisitiza Serikali kuendelea kutoa Mafunzo ya Uzoefu Kazini kwa Vijana


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, amesema serikali imeendelea kuwapatia mafunzo ya uzoefu kazini vijana ikiwamo wanaohitimu masomo yao nje ya nchi.

Ofisi hiyo kupitia Kitengo cha Huduma za Ajira (TAESA) kimekuwa kikiratibu utoaji wa mafunzo ya uzoefu kazini kwa vijana wakati wakisubiri ajira.

Prof. Ndalichako ameyasema hayo Aprili 24, 2023 alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti maalum, Mhe. Fakharia Shomar Khamis.

Katika swali lake, Mbunge huyo amehoji serikali inawatengenezea mazingira gani vijana waliofadhiliwa masomo nje ya nchi pindi wanapohitimu ili waishi maisha bora.

Akijibu swali hilo, Mhe. Waziri Ndalichako amelihakikishia Bunge serikali imeendelea kutoa ajira kupitia sekretarieti ya ajira na sekta binafsi ambayo inakua kwa kasi kubwa huku ikitengeneza mazingira ya kuwapatia mafunzo ya uzoefu kazini.