Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Serikali itaendelea kusimamia utendaji Mifuko ya Hifadhi ya Jamii - Mhe. Katambi


Serikali itaendelea kusimamia kwa karibu utendaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili kuondoa vikwazo na kuwalipa wastaafu mafao yao kwa wakati.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi, Machi 5, 2025 Bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Stella Simon Fiyao (Mb Viti Maalum) lililohoji Je, kwa nini Wastaafu hawapewi haki zao mara tu wanapostaafu?.

Akijibu swali hilo, amesema Suala la ucheleweshaji wa malipo ya mafao kwa wastaafu katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa sasa limekuwa historia ambapo Mifuko imeboresha mifumo ya TEHAMA, hatua ambayo imeiwezesha kulipa mafao ya wastaafu ndani ya kipindi kilichowekwa kisheria, au muda mfupi zaidi.