Habari

VIJANA WAHIMIZWA KUCHANGAMIKIA FURSA ZA KIUCHUMI

VIJANA WAHIMIZWA KUCHANGAMIKIA FURSA ZA KIUCHUMI

Vijana nchini wamehimizwa kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo katika maeneo yao ili kuweza kubuni miradi itakayowawezesha kujikimu na kuchangia maendeleo ya nchi yao.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipotembelea kikundi cha vijana cha bustani ya mbogamboga katika Kata ya Kiomonimkoani Tanga Octoba 11, 2018 na kueleza kuwa asilimia 56% ni vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa, hivyo wanapaswa kuchangamikia fursa mbalimbali zilizopo nchini ili kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira.

“Vijana hawa wakitengenezewa mazingira wezeshi na kupatiwa ujuzi wataweza kujiariji na kuajiri wenzao kwa kufanya kazi zenye staha zitakazo wawezesha kujipatia kipato.” alisema Mhagama

Aliongeza kuwa, Serikali imeendelea kuwajali vijana kwa kutoa mikopo kote nchini kupitia vikundi mbalimbali vya vijana kulingana na miradi wanayotekeleza, hivyo watumie fursa hiyo kwa kupata mitaji itakayowawezesha kuanzisha miradi itakayowakomboa kiuchumi.

Aidha, Waziri Mhagama aliwapongeza vijana kwa uamuzi na ubunifu waliochukua katika kuanzisha mradi huo na alitoa rai kwa vijana wote nchini kuacha kukaa vijiweni na badala yake watumie muda wao kujishughulisha na kuwa chachu ya maendeleo ya taifa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela amewataka vijana kuungana na kuwa chazo cha mabadiliko ya kiuchumi kwa kuachana na tabia ya kufanya kazi za zisizo na malengo na kuwasisitiza kutambua kuwa wanamchango mkubwa katika maendeleo ya nchi.