Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ndalichako atoa rai kwa mashirika ya Umma na Binafsi kuwawezesha vijana wajasiriamali


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako ametoa rai kwa mashirka ya Umma na Binafsi kuendeleza utaratibu wa kuwawezesha vijana wajasiliamali kufanya biashara zao kwa ufanisi ili kujenga jamii yenye usawa wa kuchochea uchumi nchini.

Ameyasema hayo wakati wa hafla ya Ushirikishwaji na Uwezeshaji vijana kiuchumi kupitia Programu ya Chipsika kiajira na Coke iliyoandaliwa na kampuni ya Coca-Cola kwanza ambayo ni Kampuni tanzu ya Coca-Cola Beverages Afrika kwa kushirikiana na Taasisi ya Ustawi wa Jamii, tarehe 29 Oktoba, Jijini Dar es salaam.

Mhe. Ndalichako ametoa rai kwa wadau wengine wa maendeleo kuiga jambo hilo ambapo Kupitia program ya Chipsika Kiajira na Coke, Vijana 900 wanao jishughulisha na shughuli za upikaji wa chakula maarufu (Chips) wa Dar es Salaam wamepatiwa mafunzo ya Ujasiliamali, Uwekaji wa kumbukumbu za taarifa za biashara, Ukuzaji wa mitaji pamoja na Elimu ya saikolojia.

Aidha, Vijana hao wamekabidhiwa majiko ya gesi 300, na mitungi ya gesi yakilogramu 15 ipatayo 300, makabati ya kuweka chakula 35, Meza jumla 80 pamoja na Apron 900 zikiambatana na fulana. Vitendea kazi hivyo vinatarajiwa kuwawezesha kuongeza tija katika biashara zao

Amesisitiza kuwa serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia imendeleea kuweka Sera, Mipango na programu wezeshi za kuwainua Vijana nchini ikiwa ni pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao hadi sasa tayari umewezesha kutoa mikopo ya Shilingi bilioni 8.13 kwa zaidi ya vijana 1,057.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Coca-Cola Kwanza, Unguu Sulay, amebainisha kuwa kamuni hiyo imekuja na mpango huo kabambe wenye lengo la kwenda kutambua juhudi zifanywazo na vijana nchini ili kuwajengea uwezo vijana wajasiliamali wa chakula ili kuweza kuongeza ufanisi wa shughuli zao.

Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni amebainisha kuwa Taaisi hiyo inaendelea kutekeleza dhima ya chuo hicho ya kuleta ustawi wa Jamii ambao utawezesha namna bora ya kuwezesha jamii yenye usawa wenye kuchochea Maendeleo nchini