Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ndalichako "Vyuo zingatieni Mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi "


Serikali imevitaka vyuo kuzingatia mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi ili kuondoa malalamiko kutoka kwa waajiri kwamba wahitimu wengi wanahitimu bila kuwa na ujuzi unaohitajika kwenye soko la ajira.

Hayo yamesemwa leo tarehe 12 Novemba, 2022 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako Mb) alipomuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kwenye mahafali ya 57 ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salam ambapo wahitimu 1,065 walitunukiwa vyeti vya ngazi mbalimbali.

Alisema serikali katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 ilitenga Sh bilioni 9 ambazo ziliwezesha vijana zaidi ya 62,000 kupata mafunzo ya uanagenzi na katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 kwa ajili ya kuendelea kutoa mafunzo ya uanagenzi.

Mhe. Ndalichako Amepongeza Profesa Emmanuel Mjema kwa kazi nzuri aliyoifanya akiwa mkuu wa chuo hicho kwa kipindi cha miaka 10 kwani chini yake chuo kimepata mabadiliko makubwa kitaaluma kwani alikipokea kikiwa katika hali mbaya.

Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kujali maendeleo ya wananchi kwa kuhakikisha wanapata huduma stahiki kwa kuboresha huduma vyuoni.

Mhe. Kigahe amempongeze Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu, ambaye ni mlezi wa Kampasi ya CBE kwa kukubali kutenga muda na kushiriki katika jitihada za kuchangisha fedha ili kusaidia kukamilisha ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike katika kampasi ya Mbeya.