News
Waziri Ridhiwani aipongeza CBE kwa elimu ya Biashara kwa Vijana na Wenye Ulemavu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameupongeza uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kwa kutoa mafunzo ya biashara na ujasiliamari hususani kwa Vijana na Wenye Ulemavu.
Ametoa pongezi hizo leo Novemba 16, 2024 wakati wa mahafali ya 17 ya chuo cha Elimu ya Biashara (CBE ) jijini Mwanza, ambapo amesema kuwa elimu ya biashara na ujasiriamali itawasaidia vijana kushiriki kikamilifu katika kukuza maendeleo ya uchumi na viwanda .
Aidha, Mhe. Ridhiwani amebainisha kuanzishwa masomo kwa njia ya Uanagenzi kwa wanafunzi jambo ambalo litasaidia vijana kumudu soko la ajira.
Ametoa rai kwa Taasisi za Umma na binafsi kushirikiana na chuo hicho ili kuendelea kukuza uchumi na maendeleo ya Taifa.