News
Waziri Sangu akagua Mradi wa ujenzi wa Ukumbi wa Mkutano Mount Kilimanjaro Convention Centre (MK-CC)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, leo Mei 16, 2026 ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi mkubwa wa mikutano wa Mount Kilimanjaro Convention Centre (MK-CC) jijini Arusha, unaotarajiwa kuwa miongoni mwa kumbi za kisasa zitakazochochea ukuaji wa sekta ya mikutano na utalii nchini.
Katika ziara hiyo, Mhe. Sangu aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Fortunatus Magambo.
Aidha, PSSSF ndiyo msimamizi wa utekelezaji wa mradi huo unaojengwa na kampuni ya China Railways Construction Engineering Group.
Ukumbi huo wa kisasa unakadiriwa kubeba zaidi ya watu 5,000 kwa wakati mmoja, hatua inayotarajia kuifanya Arusha kuwa kitovu kikubwa cha mikutano na matukio ya kimataifa Afrika Mashariki.
