News
Waziri Sangu: Tushirikiane Kuimarisha Mahusiano
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu amehamasisha Taasisi na Viongozi wa Dini nchini kuendelea kushirikiana na Serikali ili kukuza mahusiano.
Aidha, amesema Ofisi ya Waziri Mkuu imepewa dhamana ya kuratibu masuala ya mahusiano nchini baina ya Serikali na makundi mbalimbali ya kijamii ili kuendelea kudumisha tunu za Taifa ambazo ni Amani, Upendo, Mshikamano na Umoja wa kitaifa kwa ustawi na maendeleo ya Taifa.
Waziri Sangu amesema hayo leo (Jumapili, Aprili 12, 2026) alipomwakilisha Waziri Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba, katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la Parokia ya Mt. Fransisco wa Asiz iliyopo Msandamungano, mkoani Rukwa.
Katika harambee hiyo, Mhe. Sabgu amefanikiwa kuchangisha zaidi ya Tsh. Milioni 53,000,000 ambapo katika pesa hiyo Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amechangia Tsh. Milioni 20 taslimu.
Amesema, Serikali inatambua mchango wa Taasisi za Dini katika kuletea Taifa maendeleo.
"Dhamira hii imedhihirishwa kwa vitendo katika kushitikisha Taasisi za Dini katika kuandaa, kukamilisha hafi kuzindua Dira ya Maemdeleo 2050 ambayo imebeba maono ya pamoja ya kuijenga Tanzania tuitakayo," amesema Waziri Sangu.
Vilevile, Mhe. Sangu amesema Serikali imeendelea kushirikiana na Taasisi na Viongozi wa Dini ikiwemo kuchangia shughuli za ujenzi na maemdeleo ya taasisi za dini, hivyo amewasihi waumini wa dini mbalimbali kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea Maendeleo Watanzania.
Kadhalika, Waziri Sangu alitumia fursa hiyo kuwahamasisha Viongozi wa Dini kuendelea kuwalea kiroho vijana ili waendelee kuwa na maadili, tabia njema, wazalendo na kuwa na jamii tulivu yenye amani.
Kwa upande mwengine, amemshukuru Baba Padri Didas Aisakus Nandi, Paroko wa Parokia ya Mt. Fransisco wa Asiz na wanakamati kwa kuratibu vizuri zoezi la harambee ya ujenzi wa Kanisa la Parokia ya Mt. Fransisco wa Asiz.
Awali akisoma risala kwa Mgeni rasmi Katibu wa Ujenzi wa Kanisa hilo Jofrey Karinji, amesema jumla ya Tsh. Milioni 900,000,000 zinahitajika kukamilisha ujenzi huo ambapo Tsh. Milioni 200,000,000 zimeshatumika kwa hatua za awali.
Kwa upande wake Padri Didas Aisakus Nandi, Paroko wa Parokia ya Mt. Fransisco wa Asiz na Mwenyeji wa shughuli ya Harambee, ameonesha dhamira thabiti ya kuendelea kushirikiana na Serikali katika kujenga na kudumisha mahusiano mema yenye kuleta mshikamano wa kijamii.
Aidha, amesem Kupitia juhudi zake za kiroho na kijamii, ataendelea kuwa kiungo muhimu kati ya waumini na mamlaka za Serikali, akihamasisha ushirikiano, amani na maendeleo endelevu.

