Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kamati ya Bunge yaridhia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu 20244/2025


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeridhia Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Aidha, Kikao cha kamati hiyo kimefanyika leo Machi 21, 2024 bungeni jijini Dodoma kikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq ambapo ameipongeza Wizara hiyo kwa kuandaa bajeti ambayo itawezesha utekelezaji wa majukumu sambamba na kuleta mageuzi katika sekta ya Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu.

Katika kikao hicho Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameongozana na Naibu Waziri wa ofisi yake Mhe. Patrobas Katambi pamoja na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mhe. Mhandisi Cyprian Luhemeja kuiongoza menejimenti na Wakuu wa taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo kuwasilisha bajeti hiyo.