Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kamati ya Bunge yashauri bajeti Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iongezwe


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeshauri Serikali iongeze bajeti ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili kufikia malengo na tija iliyokusudiwa ya kuwainua vijana kiuchumi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq (Mb) ametoa ushauri huo leo Februari 7, 2024 alipokuwa akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2023.

Amesema kuwa, ufinyu wa bajeti
umepelekea mfuko huo kushindwa kukidhi mahitaji ya utoaji mikopo kwa vijana.

Pia, Kamati imeshauri Serikali kuunganisha mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili kuwa na tija endelevu ya kuwezesha vijana kimitaji.