Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Katibu Mkuu Luhemeja apongeza ubunifu na weledi Menejimenti Ofisi ya Waziri Mkuu


KATIBU MKUU LUHEMEJA APONGEZA UBUNIFU NA WELEDI MENEJIMENTI OFISI YA WAZIRI MKUU

Na. Mwandishi wetu – Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja ameipongeza Menejimenti ya Ofisi hiyo kwa kuendeleza ubunifu na weledi wenye kulenga mageuzi yenye tija katika sekta ya Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu nchini.

Mhandisi Luhemeja ametoa pongezi hizo leo Februari 1, 2024 wakati wa kikao cha utekelezaji wa randama ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Aidha, kikao hicho kimehudhuriwa na Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo ikiwemo Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).