Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Katibu Mkuu Prof. Katundu awaongoza Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kushiriki JKT Marathon


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu amewaongoza watumishi wa wizara hiyo kushiriki mbio za JKT Marathon KM 21 zilizoandaliwa na JKT.

Mbio hizo zimefanyika Juni 25,2023 Jijini Dodoma ikiwa ni Miaka 60 tangu kuanzishwa Kwa JKT.

Katibu Mkuu Prof.Katundu amewahimiza watumishi hao kuwa na desturi ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara yatakayo wasaidia kuwa watumishi wenye Afya njema na kuweza kuwatumikia watanzania kwa kuwawezesha kuwa na jamii yenye mahusiano mema mahali pa Kazi, nguvu kazi shindani na maisha bora.

Mgeni rasmi alikuwa ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliyeambatana na viongozi wengine akiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson, Waziri wa ulinzi Mhe. Innocent Bashungwa na viongozi wengine.

Mbio hizo zimebeba kaulimbiu isemayo “Malezi ya Vijana, Uzalishaji mali na Ulinzi kwa Ustawi wa Taifa.