Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

MAWAKALA WA AJIRA BINAFSI WA TANZANIA, QATAR WAJADILI FURSA ZA AJIRA


Mawakala wa ajira katika sekta binafsi nchini Tanzania wamekutana na kujadili fursa za ajira na Mawakala wenzao wa ajira binafsi wa Qatar, Jijini Doha tarehe 30 Agosti, 2022.

Mawakala hao wameongozana na Ujumbe wa Serikali ya Tanzania ulioongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu.

Katibu Mkuu Prof. Katundu amesema Tanzania inajivunia kuwa na vijana wenye ujuzi na uzoefu katika fani mbalimbali hivyo wanaamini kuwa endapo vijana hao watapatiwa fursa za ajira nchini Qatar watasaidia kuboresha zaidi uchumi wa Qatar pamoja na Maisha yao.

“Lengo kubwa la kuwakutanisha mawakala wa ajira binafsi wa Tanzania na wa Qatar ni kufahamishana taratibu za ajira kwa pande zote mbili ili kuweza kufanya kazi kwa ushirikiano na kupata waajiriwa wenye sifa stahiki”

Awali, akifungua mkutano huo, Mkuu wa Kitengo cha Uratibu kutoka Wizara ya Kazi nchini Qatar, Bw. Hamad Ali Elfaifa amesema Qatar na Tanzania zina uhusiano wa muda mrefu na wa kihistoria ambao umedumu hadi sasa na wanapenda kuuendeleza kwa kushirikiana katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya ajira.

Bw. Elfaifa amewataka Mawakala wa ajira kutoka Tanzania kuzingatia sheria na taratibu za ajira pamoja na kushirikiana na Mawakala wenzao wa Qatar ili kuweza

kupata wafanyakazi wenye ujuzi, maarifa na weledi kwa maslahi ya pande zote mbili.

"Katika kutekeleza Mkataba wa Ajira kati ya Tanzania na Qatar, sasa Tanzania imeingizwa kwenye mfumo wa ajira hapa nchini, Kwa hatua hii Mawakala wa Tanzania wataweza kupokea mahitaji ya nafasi za kazi kutoka kwa Mawakala wa Qatar, hatua itakayowezesha watanzania wengi wenye sifa kunufaika na nafasi za kazi hapa nchini"

Mwaka 2014 Tanzania ilisaini mkataba wa makubaliano ya ajira na Qatar, ambapo kwa sasa Serikali ya Tanzania inaangalia namna ya kupata nafasi za ajira kwa Watanzania ili waende kufanya kazi nchini humo

ReplyForward