Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Mfumo Tariff Soko la ajira Wapongezwa


Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano imepongezwa kwa kuandaa na kutoa Mafunzo ya Mfumo wa Kitaifa wa Kielektroniki wa Taarifa za Soko la Ajira (NLMIS) ambayo yanalenga kuongeza ufanisi katika utoaji wa taarifa za ajira nchini.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki Bw. Benedict Sailes kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) leo Februari 19 ,2026 Dodoma amesema mfumo huo utasaidia Wizara na Taasisi mbalimbali kupata takwimu sahihi za ajira kwa vijana wa kitanzania hasa waliohitimu vyuo mbalimbali na utawarahisishia wawekezaji kutumia mfumo huo kupata wataalamu wanaowahitaji.

Naye Afisa Tafiti na Ubunifu kutoka Makao Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Bi. Nasra Abdul Kemibaro amesema mafunzo hayo yamewasaidia kujua takwimu sahihi za ajira kupitia miradi mbalimbali kwa kujua idadi ya wanawake na wanaume ambao watanufaika moja kwa moja kupitia Mirada ya maendeleo.

Bi. Grace Nyasoro Afisa Rasilimaliwatu Mwandamizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) akieleza kuhusu umuhimu wa mafunzo hayo alisema Mfumo wa NLMIS utazisaidia Taasisi hiyo kuwa na takwimu sahihi zilizotengenezwa kwenye miradi inayotekelezwa na TARI pamoja na washirika wake.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi Bw. Godwin Mpelumbe amewashukuru wadau walio jitokeza kushiriki na kujifunza mfumo huo ili waweze kutoa taarifa za ajira wanazozizalisha kutokana na shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Mpelumbe aliongeza kusema mafunzo hayo yalitolewa kwa siku nne na kushirikisha washiriki takribani 200 yataendelea kutolewa kwenye taasisi mbalimbali zikiwemo sekta binafsi na za umma kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kutumia Mfumo huo.

Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano kupitia Idara ya Ukuzaji Ujuzi inaratibu mafunzo mbalimbali ya kuongeza ujuzi kwa wataalam toka Wizara na Taasisi za umma na binafsi ili kuchochea kasi ya uongezaji fursa za ajira na ukuzajio kipato nchini.