Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Katambi aelezea madai ya waliokuwa wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Kilombero yalivyoshughulikiwa


Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, imebainisha namna ilivyoshughulikia madai ya maslahi ya waliokuwa Wafanyakazi wa kiwanda cha sukari Kilombero.

Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Patrobas Katambi ameyasema hayo Juni 28, 2023 alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mikumi (CCM), Mhe. Dennis Londo ambaye amehoji nini hatma ya madai ya maslahi ya waliokuwa Wafanyakazi wa kiwanda cha sukari Kilombero.

Mhe. Katambi akijibu swali hilo, amesema katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii zinaonesha kuwa hakuna madai ya mafao ya malimbikizo ambayo yapo kwa waliokuwa Wafanyakazi wa kiwanda cha Sukari Kilombero.

“Wafanyakazi wote waliofungua madai wamelipwa, iwapo kuna mfanyakazi yeyote ambaye hajafungua madai, ninashauri afungue madai yake ili aweze kulipwa mafao yake kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Mifuko zilizopo,” amesema