Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

​Mhe. Katambi: Serikali kushirikiana na Mabenki kuwasaidia Vijana Mikopo


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Patrobas amesema Ofisi hiyo itaendelea kushirikiana na Mabenki katika uandaaji wa mipango imara itayowasaidia vijana kupata mikopo.

Mhe. Katambi amebaninisha hayo Agosti 8, 2023 wakati wa hafla ya kufunga kongamano la siku mbili la vijana wa Mkoa wa Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzani Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Amesema vijana wametengenezewa mazingira wezeshi na serikali ya kujikwamua kiuchumi kupitia programu ya Taifa ya ukuzaji ujuzi.