Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Mtendaji Mkuu OSHA atembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu



✅ Apongeza Elimu ya Usalama Kazini kwa Umma

Na: Mwandishi Wetu -Njombe

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda, ametembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano katika Maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi yanayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mji Mwema, mkoani Njombe.

Bi. Mwenda, aliambatana na Kamishna wa Kazi wa Ofisi hiyo, Bi. Suzan Mkangwa , ambapo wamepokea maelezo ya kina kuhusu majukumu ya vitengo na idara mbalimbali za Ofisi hiyo.

Maelezo hayo yalijumuisha masuala ya Mahusiano Kazini, Kinga ya Jamii, Ukaguzi wa Kazi, pamoja na Huduma za Ajira.

Akizungumza mara baada ya kutembelea banda hilo, Mtendaji Mkuu huyo wa OSHA amewapongeza maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuendelea kutoa elimu kwa umma kupitia maadhimisho hayo.

“Kutoa elimu kwa umma ni hatua muhimu inayochangia moja kwa moja kuongeza uelewa wa wafanyakazi na waajiri kuhusu umuhimu wa kuzingatia usalama na afya kazini,” alisema Bi. Mwenda.

Maonesho hayo ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi yanayofanyika kitaifa kila mwaka kuelekea Mei Mosi.