Habari

NAIBU WAZIRI IKUPA APONGEZA TUZO ZA I CAN

NAIBU WAZIRI IKUPA APONGEZA TUZO ZA I CAN

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa amepongeza Tuzo za I CAN zinazoratibiwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam, Mhe. Ikupa alisema kuwa Serikali ina mpango endelevu wa kutoa elimu kwa jamii juu ya masuala ya Watu wenye Ulemavu..

''Serikali imeendelea kutoa elimu juu ya Sera, Sheria na Miongozo kwa wadau na umma kwa ujumla kuhusu masuala mbalimbali ya Watu wenye Ulemavu ili kuwa na ujumuishwaji wa kundi hilo maalumu katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na kijamii,'' alisema Ikupa


Aidha, Naibu Waziri Ikupa alimpongeza na kumshukuru Dkt. Reginald Mengi kwa moyo wake kipekee wa kutambua na kwasaidia Watu wenye Ulemavu.