Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Naibu Waziri Katambi akagua mradi wa Vijana BBT


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi ametembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Programu ya (Building Better Tommorow (BBT) katika kituo atamizi cha vijana kilichopo Chuo cha Kilimo Horti - Tengeru, mkoani Arusha.

Aidha, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu inatekeleza Programu ya kuwezesha ushiriki wa vijana na wanawake katika kilimo biashara.

Vijana 812 wanufaika wa Programu ya BBT wanaendelea na mafunzo ya kilimo biashara katika vituo atamizi 13 nchini.

Baada ya hatua ya uatamizi vijana hao wataanza kufanya kilimo biashara kupitia mashamba ya pamoja (block farms).