Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Naibu Waziri Katambi ataka Ubunifu wa Mawasiliano Ofisi ya Waziri Mkuu


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amewataka Wakuu wa Vitengo na Maafisa Mawasiliano wa Ofisi hiyo pamoja na Taasisi zake kuwa wabunifu na kuongeza wigo wa kujitangaza.

Mhe. Katambi ameyasema hayo Juni 1, 2023 jijini Arusha katika kikao kazi cha kuandaa mpango wa pamoja wa mawasiliano kati ya Ofisi hiyo na taasisi zake ambazo ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

Naibu Waziri Katambi amesema vitengo vya mawasiliano vinapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia mabadiliko ya teknolojia na kuja na ubunifu utakaorahisha kufikisha taarifa muhimu kwa umma.

Pia, ameelekeza Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo na Wakurugenzi wa Taasisi hizo kuangalia umuhimu wa kuongeza bajeti kwa vitengo hivyo ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Awali, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Said Mabie na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi hiyo, Ibrahim Hamidu wameeleza madhumuni ya kikao hicho na umuhimu wa kuwa na mpango huo katika kusaidia kuwa na uratibu mzuri wa kufikisha taarifa kwa umma.