Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

​Nimeridhishwa na Maandalizi Kuelekea Maadhimisho ya Mei Mosi - Majaliwa


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambayo yatafanyika kitaifa mkoani Singida kesho tarehe 1 Mei 2025.

Amesema hayo leo Aprili 30, 2025 wakati akikagua maandalizi hayo ambayo yatafanyika katika uwanja wa Bombadia mkoani humo.

“Nimeridhishwa na maandalizi, niwatie shime tukamilishe sehemu iliyobaki, kesho tutakuwa wote, Waziri Mhe. Ridhiwani Kikwete yupo na timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu Pamoja na wadau wa utatu kwa ajili ya tukio hili muhimu .

Mhe. Majaliwa amesema Serikali inaridhishwa na ushirikiano uliopo baina yake na vyama vya wafanyakazi nchini na itaendelea kuwajibika kwa masuala yote muhimu yanayowaguswa wafanyakazi.

Awali akitoa taarifa ya Maandalizi hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema hatua ya kukamilika kwa maadalizi hayo umefanywa na serikali kwa ushirikiana na wadau wa utatu ambao ni ATE, ILO na TUCTA.

Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.