Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Kamati ya Kudumu ya Bunge yapongeza Ufanisi wa mfumo e-Utatuzi



Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imetoa pongezi kwa Tume ya Usuluhishi na uamuzi (CMA) kwa kuanzisha matumizi ya Mfumo wa e-Utatuzi ambao umekuwa msaada mkubwa katika kuboresha huduma za utatuzi wa migogoro ya kazi.

Aidha, Kamati hiyo pia imempongeza Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha Tume ya Usuluhishi na Uamuzi fedha kwa ajili ya kuwezesha Mfumo wa Usimamizi wa Mashauri ya Usuluhishi na Uamuzi e-Utatuzi kusimikwa kwani ni utachochea uchumi wa nchi yetu kwa kuwa utasaidia kupunguza foleni za usikilizwaji wa mashauri na kuwarqhisishia wananchi wanaotoka umbali mrefu kuifuata Tume.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Hawa Mchafu ilipofanya ziara Machi 18, 2026 katika Ofisi za CMA ili kukagua Mfumo huo wa usimamizi wa Mashauri.

Awali akizungumza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri ya Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Rahma Kisuo amesema serikali ilikuja na mfumo huu kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa haki mahala pa kazi na kusogeza huduma karibu na wafanyakazi na waajiri ambao ni muhimu katika ukuaji wa uchumi hapa nchini.

Vilevile, Mhe Kisuo ameendela kwa kusema kuwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutatua changamoto hizi na Januari, 2026 Mfumo huu ulianza rasmi kwa kuzinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu.

Naye Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Mhe. Usekelege Mpulla amesema hata hivyo Tume kwa kushirikiana na Wizara wana mkakati wa utoaji wa elimu kupitia vyombo vya habari ili kuweza kuwafikia kwa urahisi wafanyakazi, waajiri pamoja na Jamii.

MWISHO